John 18:3-8

3 aHivyo Yuda akaja bustanini. Aliongoza kikosi cha askari wa Kirumi, na baadhi ya maafisa kutoka kwa viongozi wa makuhani na Mafarisayo. Nao walikuwa wamechukua taa, mienge na silaha.

4 bIsa akijua yale yote yatakayompata, akajitokeza mbele yao akawauliza, “Mnamtafuta nani?”

5 cWao wakamjibu, “Isa Al-Nasiri.”

Isa akawajibu, “Mimi ndiye.” Yuda, yule aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao.
6Isa alipowaambia, “Mimi ndiye,” walirudi nyuma na kuanguka chini!

7 dAkawauliza tena, “Mnamtafuta nani?”

Nao wakamjibu, “Isa Al-Nasiri.”

8Isa akawaambia, “Nimekwisha kuwaambia kuwa, mimi ndiye; kwa hiyo kama mnanitafuta mimi, waacheni hawa watu waende zao.”
Copyright information for SwhKC